BAADA YA KULIKOSA KOMBE LA MAPINDUZI ZANZIBAR AFISA HABARI WA SIMBA AANZA VITUKO VYAKE, KAA TAYARI ZINAANZA

Afisa Habari wa Simba Ahmed Ali ameanza michezo yake kama msimu uliopita kwa kuwaweka roho juu mashabiki wa Simba. Hii inakuja zikiwa zimesalia siku chache kuelekea kufungwa kwa dirisha dogo la usajili Tanzania ambapo kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Ahmed Ali kaandika "KAA TAYARI" na muda ni saa nne usiku. Bila shaka hapo kuna ujio wa mchezaji mwingine ambaye ni hitaji la Kocha BENCHIKHA tofauti na hapo itakuwa ni kuwakosea mashabiki wao. Ikumbukwe kuwa mpaka sasa Simba bado wanahaha kupata wachezaji wa kuipeleka timu mbali wanakohitaji kuwa ambako wao wanafikiri Yanga itawachukua muda mrefu kufika lakini kila wakitupa macho wanahisi kama vile Yanga imeshawapita na kufika huko kwenye tarajio kitu kinachowaumiza MIOYO kuanzia Uongozi mpaka mashabiki. Na ndiyo maana kila dirisha linapokuja la usajili hujikuta wanadaka Gunzi badala ya Muhindi. Macho na Masikio ya Mashabiki wa Simba kuanzia sasa ni kwenye hiyo tarehe na muda uliotajwa na Afisa Habari wao Kipenzi. #sokatalk #tuongeemichezo #sokanikazi
Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post