GNADOU JOSEPH GUEDE ATUA YANGA KUCHUKUA NAFASI YA HAFIZ KONKON

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ivory Coast Gnadou Joseph Guede kajiunga na timu ya Yanga akitoka timu ya Tuzlaspor ya Uturuki. Gnadou Joseph mwenye umri wa miaka (29)anachukua nafasi ya Hafiz Konkon ambaye kashindwa kufikia matakwa ya timu ambayo ni kufunga magoli. Mchezaji huyu amewahi kupita kwenye Timu ya Morrison ya FAR Rabat kisha akatolewa kwa mkopo katika timu ya Emirates Club ambako hakudumu kwa muda mrefu akarejea tena FAR Rabat ambao waliachana naye ambapo alitimkia Uturuki katika timu ya Tuzlaspor aliyoichezea michezo minne ambayo hakubahatika kupata bao hata moja.
Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post