HADITHI:ZAWADI YA UPENDO (Hadija Salumu)


HADITHI: ZAWADI YA UPENDO 

SEHEMU YA KWANZA 

MTUNZI: HADIJA S. MGAZA 

MAWASILIANO :.. 0678204094 (WhatsApp) 


TUNAANZA... 

"Mkewangu amka ..."

Aaah..jamani nimechoka mwenzio....!

"Jikaze mkewangu ..

"Jamani .baby acha buana nilale ata kidogo ..!

"Unajua saizi saa ngapi?

"Aah...mi ata sijui buana ..!

"Saizi saa mbili kasoro ..ujue 

"Khaa kumbe ..ngoja niamke hivyo hivyo..!

Anaitwa munira ..akiwa na mmewake wakuitwa Adnani Ni mke na mume 

Munira aliamka na kutoka nnje 

"Khee we bibie ..saizi ndo umeamka ..

"Shikamoo mama ..!

"Kua upate yako ..alaah..

Mwanamke gani unakua mvivu hivyo ...

Huyo Ni mama wa Adnani

"Jamani mama ..nilipitiwa tu mie.

"Kwaiyo unategemea Nani akufanyie kazi ?

"Hapana mama ..

"Mama kwani Kuna nini?

"Yani huyu mwanamke ana lala mpaka saizi ..anategemea kazi amfanyie Nani ?

"Mama ..mbona hivyo ? 

Kwani kila siku anaamka muda Kama ..huu ?

Mbona unakua hivyo mama yangu 

"Kwaiyo we unaona sawa.mkeo kuamka saa mbili?

"Sio hivyo mama ..munira ana jisikia vibaya hajalala usiku mzima 

Siunajua anaumwa lakini ?

"Adnani embu acha kubishana na mama ..embu nenda kazini ..tuta onana badae ..!

Munira aliingilia kati

"Mama mi naenda lakini naomba uwache kugombana na mkweo ...

Adnani akaondoka zake ...

"Mama NAOMBA unisamehe ..nimekosa Mimi sirudii Tena ...

"Nyoooo ..embu nitokee hapa ..kazi hiyo hiyo ya uvivu. ..embu toka mbere yangu nisije kufanya vibaya bure ..!

Munira aliingia jikoni na kutoa vyombo vichafu na kwenda kuosha 

....

"Daaah..nimepatikana Muni mie ..ata sijui kwanini nilimpenda huyu mwanaume ..laiti Kama sio kupenda ..saizi nisinge gombezwa na huyu mama ..nisinge kuepo hapa ..lakini ndo Nisha ya vuria nguo maji ..inanibidi niyaoge tu haina jinsi ....

Baada ya kuosha vyombo ..munira alielekea jikoni na kuchemsha chai ..Kisha akaweka mezani ...

Akaenda aliko mama mkwe wake 

"Mama chai tayari ..

"Sawa.. umewaamsha hao mawifi zako ?

"Hapana ..

"Sa unasubili Nini ..?

"Mama naenda ..niliamua nikwambie wewe kwanza ..!

"Kwaiyo unaniambia au unanishushua?

"Jamani mama ....!

"Wee mtoto koma kabisaaa sitaki kubishana na mtoto anae nuka maziwa...kwanza Ata sijui huyu Adi kakupendea Nini wewe ..?yani sikupendi we mtoto ..hee mungu mwenyewe ndo anajua ..

Munira aliumia Sana alikimbia ndani kwake na kujifungia Kisha akaanza kulia ...

"Mungu ..!kosa langu Nini mie . ee

Kwanini lakini ..mbona Mimi tu .. aaahaaa 😭😭...

Nimechoka kwa kweli yani ata sijui Nini nimemkosea huyu mama jamani..?.

Kosa langu kukubari ujio wao hapa kwangu au?

Munira akiwa anaendelea kulia 

Mala akasikia sauti..

"Hivi wewe mtoto .kwanini unakua na dharau hivyo..we sinimekwambia ukawaite wanangu ..

Munira akatoka na kuelekea kwenye mlango akaufungua na kuingia ndani ..na kukuta mawifi zake wamelala tu ..

Akasimama na kuwaangaliaaa 

Kisha akawaita ..

"Wifi zuhura amkeni mkanywe chai.!

"Aaah..we nawe mbona msumbufu hivyo ...aaaa.

"Jamani wifi..Ni chai 

"Bwana ee embu nenda huko usitupigie kelele hapa 

Munira alitoka 

"Mama we endelea kula zuhura na Zahara bado muda wao wakula.. 

Mama hakuongea kitu Bali aliwafata wanae ..

Hao watoto sio useme wadogo ..hapana ..Ni wa dada wa kuolewa kabisa ..na nimapacha 

Zuhura na Zahara

Lakini ndo hivyo ..kumtesa wifi yao ndo wanacho jua wao ..

"Nyie amkeni tukale buana 

"Mama nawe ..mbona msumbufu hivyo?

"Basi sawa wanangu .nyie laleni tu 

Nitakuja kuwaamsha baadae ...

Yule mama alienda kula ..

Baada ya mda yule mama alimaliza kula na kumuita munira

"We mtoto embu nnjoo utoe vyombo ..!

"Sawa mama nakuja 

Alisema munira na kuelekea aliko itwa 

Munira litoka vyombo na kwenda kuvisuuza ...

Baada ya mda kidogo Tena .. 

"Wifiii......

Aliita zuhura

"Nakuja...

Munira alifika ...

"Tunaomba chai 

"Jamani wifi yangu ..chai yote mpaka niwatengee kweli?

"He he he he..wewe Nani kakufundisha kutupinga?

"Wifi yangu mbona hivyo lakini ..Basi sawa mi sipendi kuongea hata kidogo ..

Munira aliongea huku akitenga chai 

Munira Alisha zoea maneno ya mawifi zake ..hasa zuhura

Munira alienda kuandaa chakula Cha mchana ...akiwa anahangaika kupika mala akasikia sm yake inaita ..

Alikua Ni mmewe

"Hello

"Vipi . mkewangu 

"Poa nambie ..

"Safi tu vipi umekula?

"Ndio mume wangu ..vipi wewe umekula?

"Ndo nataka kula hivyo na ndomaana nikakupigia sm

"Basi kula Sasa Mimi tayari 

"Sawa mkewangu ..vipi hao ndugu zangu ..bado wanakusumbua ..!

"Yaache hayo buana mi nipo nao poa tu ,,,

"Sawa 

Kabla simu haijakatwa sauti ilisikika ....



******Itaendelea*******




Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post