JIFUNZE KUTENGENEZA SABUNI YA MCHE



 Sabuni ya mche imekuwa ikitumiwa sana na jamii kubwa ya Watanzania hasa waishio Vijijini. Sabuni hii inasaidia sana hasa kwa familia za Uchumi wa kati zaidi wa chini kwa kufulia, kuogea na kuoshea vyombo na hii ni kutokana na bei yake kwa kipande. Lakini wengi wamekuwa wakijiuliza sabuni hizi hutengenezwa namna gani?

Na mimi nimeona nikupeleke darasani ujifunze kuitengeneza hii sabuni hata ukiwa sebuleni kwako.

TUANGALIE MAHITAJI YAKE 

Ili uweze kutengeneza sabuni hii unatakiwa kuwa na Mali ghafi zifuatazo :-

🔹MAFUTA

🔹MAJI YASIYO NA CHUMVI

🔹CAUSTIC SODA

🔹SODIUMSILGET

 MAFUTA haya ni yale ambayo huganda kama vile ya MAWESE, NAZI, NYONYO, Bila kusahau mafuta ya wanyama.

SODIUM SILGET ni kemikali ambayo hutumika kuondoa muwasho wa CAUSTIC SODA na kuleta umafuta kwenye Sabuni yako pia kuifanya kuwa ngumu.


NAMNA YA KUTENGENEZA SABUNI 

Chukua Sodium Sillget na iweke ndani ya Caustic Soda polepole ukikoroga mpaka mchanganyiko uwe mzuri. 

Chukua mchanganyiko wako na taratibu anza kumimina kwenye ndoo ya mafuta taratibu huku ukikoroga. Kisha mimina huo uji mzito kwenye boksi na acha ipoe kwa muda wa masaa 6 hadi 8. Baada ya kukauka toa kwenye boksi/mody kisha kata miche yako na gonga mhuri kwenye kila mche kama utahitaji kufanya hivyo. Na hapo sabuni yako itakuwa tayari kwa matumizi.

Kwa leo niishie hapo tukutane katika somo lijalo.


Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post