KENGOLD FC INAZIDI KUKIMBIZA CHAMPIONSHIP BAADA YA MICHEZO 17

Timu ya Soka ya Kengold ya mkoani Mbeya katika wilaya ya Chunya inayomilikiwa na Mwekezaji Mzawa wa Madini ya Dhahabu na Mmiliki wa Shule ya Pre & Primary School ya Kengold ya Wilayani aitwaye Kenneth inazidi kung'ang'ania namba moja ikijikusanyia pointi 39 ikiiacha timu ya soka ya Pamba ya mkoani Mwanza kwa pointi 2 yenye pointi 37 huku kila timu ikiwa imecheza michezo 17. Na kwenye msimamo huo timu ya zamani ya Afisa Habari Masau Bwire Ruvu Shooting ikiburuza mkia ikiwa na pointi 3 tu na haijabahatika kushinda mchezo hata mmoja katika michezo hiyo 17. Unafikiri timu ya soka ya Kengold itasalia hapo juu mpaka mwisho wa michuano au ni nguvu ya soda? Toa maoni yako.
Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post