Mwana Sanaa wa Filamu na Tamthilia kutoka Tanzania maarufu kwa jina la Mswahili Madebe Lidai kajitokeza na kujibu tuhuma zilizoibuliwa na mke wake Chanuo kupitia Vituo mbalimbali vya habari. Na haya yalikuwa maneno yake.. "Chanzo kikubwa cha ugomvi wetu na Chanuo ni kwamba alikuwa anawapeleka watoto wangu kwa mashoga, yani wanaume ambao (wamelefti group) mimi nawapenda sana wanangu kwahiyo sikukubaliana na hilo nikampa onyo aache kuwakutanisha wanangu na hao mashoga zake, lakini yeye alilichukulia hilo tofauti akaona kama namnyima uhuru wa kwenda kucheza na marafiki zake"
"Mimi ndiye nimeitengeneza brand ya Chanuo, kuanzia jina, account yake ya Instagram mpaka umaarufu kwa kumshirikisha kwenye movie zangu, sasa anaposema nimeishikilia account yake ya Instagram wakati mimi ndiye niliyeitengeneza na kumbrand watu wakamjua hapo kwakweli mimi nashangaa. Kwahiyo ni hayo tu yale aliyosema yote ni uongo"- Madebe Lidai