MANGE KIMAMBI KUMTAFUTIA MKE DIAMOND PLATNUMZ

Baada ya kile kinachoendelea kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kumhusu Diamond Platnumz akidai kuwa kwa sasa hana mke wala mahusiano na mwanamke yoyote yule na kuomba asihusishwe na mwanamke yoyote mpaka pale ambapo yeye atatakiwa kufanya hivyo kama ambavyo amekuwa akifanya kila wakati. Ndipo Mwanadada maarufu nchini Tanzania ambaye makazi yake ni nchini Marekani lakini akijizolea Umaarufu mkubwa nchini Tanzania kutokana na Ufukunyuku wake kwa Watu Maarufu na Viongozi mbalimbali wa Serikali hasa ya Tanzania alipoibuka na kuibeba shughuli hii yeye akiihusisha na kuachwa kwa Mwanamuziki ZUCHU ambaye kumekuwa na maneno ya hapa na pale kuwa kwenye mahusiano na DIAMOND PLATNUMZ japo wao hawajawahi kuthibitisha hilo lakini mazingira ndiyo yaliyowafanya watu wapigie mstari kuwa ni wapenzi. MANGE KIMAMBI yeye kanyoosha rula na kumuelekea ZUCHU kuwa kaachwa baada ya hiki alichokiandika DIAMOND PLATNUMZ, ameandika haya... "Jamani amkeniii, mnalala mna hela?? Mnalala mna umeme?? Amkeniiiiiiii.... Mzanzibary dawa zimeisha nguvu.... Nyie uchawi una mwisho... Nyambaf cheza na mama Dangote wewe? asipokutaka huwezi kutoboa.... ..mbav shobo zote zile kwa kina Tifa na chini kapigwa. Ametumika ka jinga kurekodi Young famous and African alafu limepigwa chini. Kama namuona huko anavyokusanya mawe aruke geti akavunje vitu 🤣🤣🤣🤣🤣 @diamondplatnumz Mdogo wangu kuanzia leo mi fan wako. Jamani usiniangushe ukarudi kwa king'ang'a maana nitalia mpaka kwikwi... Usirudi kule mdogo wangu... Jamamke chawi liwe... Kweli wee Diamond Platnumz unatokaje na kile kituko hata nimekishinda tako? Lilikuloga lile janamke mdogo wangu na umechomoka sababu mamako nae fundi... Sasa tulia mdogo wangu mi ntakupa mwanamke wa hadhi yako, yani mwanamke ambae ukitoka nae watu wanatetemeka sio lile li Zanzibar ukitoka nalo watu wanashindwa kutofautisha nani mwanamke nani mwanaume kati yenu. Mwanamke gani yule hana tako, hana nyonyo hana sura kila kitu kanyimwa? Tulia hapo hapo mdogo wangu nakuletea bonge la demu mpaka wenzio kina Kiba na Harmo wakuonee wivu... King'ang'a alikushushia hadhi mno mpaka ukaonekana huna hela ndo maana huwezi kuwa na demu mkali umelishwa kombe la Unguja... @diamondplatnumz Gazeti hili nimeandika alafu urudiane na king'ang'a haki utakuwa umenivua nguo. Ntalia mpaka nitambae chini.... Mdogo wangu soma dua kila wakati kuanzia usiku huu maana king'ang'a lazima akamlilie mamake, watakusomea makombe ya Pwani mpaka urudi bila kujijua imerudije. Soma dua. . . Now it make sense why Aaliyah kaalikwa shughuli ya kesho, nilijua tu Dai ndo kamwambia Manara amwalike. Haya Ndio mambo niyapendayo mimi.. Nyieeeeeeee!!!! . . Nyambaf king'ang'a ukamchamba dada wa Taifa kisa Rouhy, Rouhy my foot!! Sasa tunae na tunatamba nae, kimekuramba." Mwana dada MANGE KIMAMBI akawa amehitimisha hivyo gazeti lake kama alivyoliita mwenyewe. Swali ni je atamtafutia kweli? Na vipi kuhusu ujumbe huu wa Diamond Platnumz una uhalisia wowote? Au ni maandalizi ya ngoma mpya.
Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post