MJUE MCHUNGAJI UWEZA KASUNGA

Anaitwa Mchungaji Uweza Kasunga mzaliwa wa mkoa wa Mbeya katika wilaya ya Chunya katika mji mdogo wa Chalangwa. Chalangwa ni mji wa kwanza kabisa unapoiacha wilaya ya Mbeya Vijijini na kuingia wilaya ya Chunya. Hapo ndipo alipozaliwa kwa wazazi wake ambao shughuli zao kuu ni kilimo na Uchimbaji wa madini. Mchungaji Uweza Kasunga baada ya kuhitimu kidato cha nne tu alijikuta anapata wito wa kumtumikia Mungu na ndipo alipowasilisha wazo lake kwa wazazi wake ambao mwanzoni ni kama hawakumuelewa lakini baadaye walimuelewa na kumpa baraka zote na hapo Uweza alimfuata Mchungaji wake mlezi ambaye hakuwa na pingamizi lolote. Kwa ufupi hii ndiyo Historia fupi ya safari ya Mchungaji Uweza Kasunga. Historia kamili inakuijia hivi karibuni.
Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post