MSIMAMIZI NA MWANASHERIA WA CHASAMBI AMUIJIA JUU SHAFFII DAUDA

Baada ya andiko la Shaffii Dauda kumhusu mchezaji mpya wa Simba Ladack Chasambi kumshangaa kumwaga wino Msimbazi ilhali yeye alimtafutia timu Ulaya. Msimamizi na Mwanasheria wa mchezaji huyo kajitokeza na kusema kuwa baada ya yeye Shaffi kumfuata mteja wake kuhusu hilo dili la Ulaya walimtaka aweke OFA mezani ili wajue nini kinakwenda kufanywa na mteja wake huko ugenini lakini Shaffii Dauda hakufanya hivyo, wao ndipo walipompeleka Simba Sports Club baada ya kupokea OFA ambao ni nzuri. Anaendelea kufunguka kuwa baada ya mteja wake kujiunga na Timu ya Simba ndipo alipojitokeza na kuanza kumsema vibaya kwenye vyombo vya habari kitu ambacho si kizuri. Kayasema hayo wakati akihojiwa na @wasafimedia
Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post