WENYEJI WALIODHARAULIWA, Ivory Coast usiku wa kuamkia leo wamefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kutoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Nigeria katika mchezo wa Fainali Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara Jijini Abidjan.
Nahodha na beki, William Troost-Ekong anayechezea PAOK ya Ugiriki alianza kuifungia Nigeria dakika ya 38, kabla ya kiungo wa Al Ahli ya Saudi Arabia, Franck Yannick Kessié kuisawazishia Ivory Coast dakika ya 62.
Aliyewahakikishia Ivory Coast taji la kwanza ka AFCON tangu mwaka 2015 ni mshambuliaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, Sébastien Romain Teddy Haller aliyefunga bao la ushindi dakika ya 81.
Kwa ujumla hilo linakuwa taji la tatu la AFCON kwa Tembo pamoja na lile la mwaka 1992.
William Troost-Ekong wa Nigeria amekuwa Mchezaji Bora wa Mashindano, huku Ronwen Williams wa Afrika Kusini akiwa Kipa Bora na Mfungaji Bora ni Emilio Nsue Lopez wa Guinea-Bissau.