CBE YAIVUSHA YANGA HATUA YA MAKUNDI KWA KWA KIPIGO CHA MBWAKOKO



MABINGWA wa Tanzania, timu ya Yanga wametinga Hatua ya makundi ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya timu ya Benki ya Biashara Ethiopia, CBE SA (Commercial Bank of Ethiopia Sports Association) ndani ya Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Katika mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora, mabao ya Yanga yamefungwa na Mzambia, Clatous Chama dakika ya 35, Mtanzania Clement Mzize dakika ya 46, Mburkinafaso Stephane Aziz Ki dakika ya 74 na 90’+3, Mtanzania Mudathir Yahya dakika ya 88 na Mkenya Duke Abuya dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo, Yanga inafuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla wa 7-0 kufuatia kuichapa CBE SA 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita bao la Mwana Mfalme Prince Dube dakika ya 45’+1 Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa.

Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post