TK MOVEMENT YAENDELEA KUPANUA WIGO WA FURSA ILI KUTIMIZA MALENGO


 VIONGOZI TK TAIFA WAENDELEA KUPANUA WIGO WA FURSA ILI KUTIMIZA MALENGO YA TK.


Kama ilivyo moja ya malengo mahususi ya TK Movement ni kuwaunganisha Vijana na Wanawake katika fursa mbalimbali ikiwemo kuzitafuta, kushiriki, na kujifunza namna ya kuzinyakua fursa hizo ndani na nje ya Tanzania.


Mapema leo Tarehe 17 Oktoba, 2024 Viongozi wa TK Taifa Mratibu Mkuu kushoto na Mkuu wa Idara ya TEHAMA kulia wameshiriki Mkutano Mkuu wa Benki ya Ushirika Tanzania uliofanyika Jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Wa Kilimo, hii ikiwa ni sehemu moja wapo ya kuendelea kufungua, kujenga mahusiano na kuzikaribisha fursa mbalimbali zitakazopatikana ili kuweza kuwanufaisha Vijana wa Kitanzania ndani ya TK.


TK Movement tunasema tutaendelea kuwa kiungo na daraja muhimu kati ya Vijana, Wanawake na Serikali ili kuwa na Taifa bora na imara.


Imetolewa na TK MOVEMENT Tanzania 


#tkmovement

#SSH

#MamaYetuTaifaLetu.

#TaifaLetuKeshoYetu.

#UchaguziSerikaliZaMitaa2024

Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post