Marekani iko vitani na Nyoka wa Mti wa Brown, ambaye ana urefu wa mita tatu hivi. Inagharimu dola milioni nane kwa mwaka.
Inashangaza kwanini serikali ambayo inastahili kulinda wanayama pori inaua nyoka huyu. Marekani inasema imechukua hatua hiyo kutokana na uharibifu unaofanywa na nyoka huyo.
Nchi hiyo imetumia miligramu 80 ya paracetamol kuua nyoka hao kisiwani Guam.
Nyoka hao ambayo huishi kwenye miti hula panya walionaswa kwenye magamba ya miti. Paracetamol ikitumiwa kwa panya kama mtego huua nyoka ndani ya saa chache.
Idara ya Kilimo ya Marekani inatumia vifaa maalum kufuatilia baadhi ya panya ili kubaini ikiwa nyoka wamekufa kutokana na kula paracetamol.
Kisiwa cha Marekani cha Guam kipo magharibi mwa bahari ya Pasifiki karibu kilomita 11,000 kutoka eneo la bara la nchi hiyo.
Kisiwa hicho kiko karibi kilomota 2,500 kutoka Ufilipino na na kilomita 4,500 kutoka Australia.
Idadi ya nyoka wa mti wa brown katika kisiwa cha Guam imeongezeka mara dufu. Nyoka hao ni tishio kwa aina ya spishiya ndege wa kipekee ambao ni nadra kupatikana.
Marekani inasema spishi tisa ya ndege kati ya 11 wameangamia kutokana na hilo. Kando na hilo maisha ya twiga na popo yako hatarini.
Chanzo: BBC SWAHILI