Chui Mweusi "Singida Black Stars" imemuuza mshambuliaji wake chipukizi, Suleiman Mwalimu Abdallah 'Gomez' kwa dau ambalo halijatajwa kujiunga na Wydad Club Athletic ya Morocco.
Mwalimu (26) anakwenda Wydad baada ya kucheza kwa mkopo Fountain Gate FC mzunguko wote wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na amefunga mabao sita na anashika nafasi ya tatu katika chatu ya wafungaji mabao mengi, nyuma ya Mkenya, Elvis Baranga Rupia nane na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua saba.
Anakuwa Mtanzania wa pili tu kuingia kwenye orodha ya wachezaji wa Wydad Club Athletic maarufu kama Wydad Casablanca baada ya kiungo mshambuliaji Simon Happygod Msuva aliyechezea timu hiyo Kati ya mwaka 2020 na 2021.
Tags:
Habari/Matukio