MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU:
1. Mtihani wa darasa la Saba utafutwa ifikapo 2027.
2. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize Kidato cha nne. Hii itaitwa Elimu ya Msingi.
3. Kutakuwa na Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa darasa la sita (STANDARD SIX NATIONAL ASSESSMENT) ifikapo 2026.
4. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza Kidato cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza. Hii itaanzia Secondary ambapo kutakuwa na mikondo miwili; Jumla na Amali.
5. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa kama somo kwa Shule za Kiswahili Medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa Shule za English Medium.
6. Elimu ya Msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6 tofauti na ya sasa miaka 7.
8. Elimu ya Awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5. Mwanzoni elimu ya awali haikuwa rasmi na shule za Serikali haikuwepo. Sasa itakuwepo kwa utaratibu huo.
9. Masomo ya Elimu ya Msingi yatakuwa ni KKK(Kusoma, Kuhesabu, Kuandika), Jiografia, kiswahili, Sanaa na Michezo, Hisabati, Sayansi, historia ya TANZANIA na Maadili, Dini na kiingereza na Stadi za Kazi itachomekwa.
10. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.
11. Shule zenye uwezo zitafundisha angalau somo moja la lugha za kigeni kama Kichina au Kifaransa.
12. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na Amali (Ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na uwezo, matakwa na malengo yake ya baadaye.
13. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani zifuatazo:-
👉Kilimo na Ufugaji.
👉Umakenika.
👉 Biashara na Ujasiriamali.
👉 Sanaa na Ubunifu.
👉 Elimu ya Michezo.
👉Ufugaji wa Nyuki.
👉 Uchimbaji wa Madini.
👉Urembo.
14. Mwanafunzi wa Mkondo wa Amali atatakiwa kuchukua Masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.
15. Masomo ya jumla ya wanafunzi wa Amali ni:-
👉 Hisabati.
👉Elimu ya Biashara.
👉Kiingereza.
👉 Historia ya Tanzania na Maadili.
16. Wahitimu wa Amali watapata vyeti viwili yaani:-
Cheti cha ujumla cha Elimu ya Sekondari (NECTA) na Cheti cha Amali ( NACTIVET).
17. Kila shule itakuwa na Wakala wa VETA ili kusimamia masuala ya Ufundi.
18. Kila shule haitakuwa na Mikondo zaidi ya miwili ya Ufundi, hii ni kwa ajili ya Ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.
19. Kutaanzishwa somo jipya la Mawasiliano ya Kitaaluma (ACADEMIC COMMUNICATION) katika A-level na Ualimu.
20. CODING itafundishwa Shule za Msingi.
21. INFORMATION and COMPUTER STUDIES (ICS) itabadilishwa na kuitwa COMPUTER SCIENCE.Somo limesukwa upya.
22. CIVICS itaunganishwa na Historia ya TANZANIA na Maadili kwa O-level.
23. O-level Masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.
24. Katika O-level Masomo ya Biology na Geography yatakuwa Masomo ya kuchagua pia kwa sababu Maudhui yake yamekuwa kwenye Masomo ya Jiografia na Sayansi ya Shule ya Msingi kwa mfano Afya ya Jamii, Afya ya Uzazi, Magonjwa ambukizi nk.
25. Civics, Maarifa ya Jamii, Uraia na Maadili yamefutwa, Maudhui yake yameingia katika somo la Historia ya TANZANIA na Maadili.
26. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na Maudhui yake yatawekwa katika Somo la Historia ya TANZANIA na Maadili na Mawasiliano ya Kitaaluma.
27. Kufuta baadhi ya Masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudiarudia kwa Maudhui.
28. Michepuo katika Elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9).
Michepuo iliyoongezeka ni:-
👉Sanaa.
👉Lugha.
👉Muziki.
👉Michezo.
👉Tehama.
29. Masomo ya O-level yatakuwa:-
👉 Biology.
👉 Physics.
👉 Chemistry.
👉History.
👉Geography.
👉 Historia ya TANZANIA na Maadili.
👉 Hisabati.
👉 Kiswahili.
👉English.
👉Elimu ya Biashara.
👉 Utunzaji wa _Taarifa za Fedha.
👉 Computer Science.
👉Bible Knowledge.
👉 Elimu ya Dini ya kiislamu etc.
30. Astashahada ya Ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (DIPLOMA) ya Elimu ya Awali, Ualimu wa Msingi na Ualimu wa Elimu Maalumu.
Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza Kidato cha Sita na itasomwa kwa miaka miwili tu.
31. Walimu wa Sekondari wote watakuwa na Shahada (DEGREE). kwa sababu nchi nyingi zinaenda na mwelekeo huu.
32. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (DIPLOMA) ya Ualimu wa Sekondari vitatumika kutoa "Continuous Professional Development."