TAIFA LETU, KESHO YETU
Jana tarehe 11/2/2025
TK Movement Mbeya mjini walipata mwaliko wa kuhudhulia Uzinduzi wa Kampuni ya DIGI-TRUCK iliyo chini ya kampuni ya simu kutoka China ya HUAWEI na Taasisi ya TULIA TRUST chini ya Mkurugenzi wake DR TULIA AKSON ambaye ni Raisi wa Mabunge Duniani (IPU)
Kampeni hii ambayo ni kama fursa ina lengo la kuisadia jamii kufahamu umuhimu na matumizi ya TEHAMA katika jamii ili kuendana na Mabadiliko ya Teknolojia katika Mapinduzi ya Kiuchumi na Kijamii.
MBEYA ni mkoa wa sita kupata bahati ya fursa hii ambapo mafunzo haya ya bure yatatolewa kwa muda wa siku Saba.
Baadhi ya Viongozi wa Mbeya Mjini na Mkoa uliwakilishwa na Mjumbe wa Idara ya Wanawake ambaye aliadhimia kwenda kuwapa Taarifa Wananchi ili wajitokeze Kwa wingi katika fursa hii lakini pia walipata wasaa wa kukutana na Makundi mbalimbali ambayo waliwapa Elimu kuhusu TK Movement.
#FURSA Haziongei Bali Mahitaji yatakufanya kuzitafuta