USIWE GUNDI, FUNGUA MLANGO WA PILI

 

Part 01
USIWE GUNDI, FUNGUA MLANGO WA PILI


Kwenye maisha yetu ya Kitanzania tunasumbuliwa na HOFU. Kwanini HOFU? Asilia kubwa ya Watanzania au Waafrika kwa ujumla hatuishi maisha yetu wenyewe bali tunaishi maishi ya kupangiwa na kutishwa na Wanafamilia hasa Walezi na Wazazi na hapa ndipo HOFU ilipozaliwa.

Mtu anawaza kuwa anachokifanya kiuhalisia hakitoki ndani yake ni matakwa ya wale waliomuwezesha kusoma mpaka kupata hiyo kazi lakini kilicho ndani yake si ile kazi bali kuna kitu kingine kabisa.
Mfano kuna mtu muda huu yuko kazini akifanya kazi yake ya Udaktari lakini ukimuuliza hii kazi ni ya Ndoto yako atakwambia we acha tu hii si chaguo langu mimi nilitamani kuwa Muongoza Watalii ila ndiyo hivyo Wazazi waliweka uamuzi.
Mtu kama huyu tunamwita ni Mfungwa wa Kazi yake na hawezi kuwa na Furaha Maishani mwake.
LA MUHIMU:
Pamoja na kile unachokifanya kwa sasa unaweza kufungua mlango wa pili ambao huo ni wa ndoto yako au kutokana na ushauri wa marafiki waliofanikiwa kufanya hicho kitu na ni miongoni mwa vitu unaona ukifanya utapata Amani ya Moyo. Na baada ya hapo utaangalia Mlango huo Umekupa Mafanikio gani, ikiwa utakupa mafanikio makubwa unaweza kuamua kuendelea na kazi ya awali au kuiacha kabisa ili upate nafasi ya kuupambania mlango wako.

Kuna watu waliamini kazi zao za awali ni za Ndoto zao na wakaweka nguvu zao huko lakini baada ya muda mrefu hawakuona Ndoto zao zikifanikiwa hivyo waliamua kufungua Mlango wa Pili ambao umewapa Mafanikio makubwa. ANGALIA, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere awali alikuwa Mwalimu lakini baada ya kufikiri kwa muda aliamua kuifuata ndoto yake kwa kufungua mlango wa pili ambao ulikuwa ni SIASA, baada ya kuingia kwenye SIASA Historia iliandikwa ikiwa ni pamoja na kuiletea Uhuru nchi yetu ya Tanzania wakati huo ikiitwa Tanganyika kabla ya Muungano na Zanzibar. Wengine ni Baba LEVO na Mwijaku walikuwa kwenye kazi ambazo waliamini ndiyo kazi za Ndoto zao lakini wapi.

Mtakumbuka Baba LEVO kafanya Muziki kwa muda mrefu lakini hakuwa na Mafanikio yoyote akaona afungue mlango mwingine ambao ulikuwa ni wa SIASA akaenda kwao Kigoma akatia Nia kwenye kiti cha Udiwani na kwa bahati nzuri alipita na kuwa Diwani, alichoambulia kwenye nafasi hiyo ilikuwa ni kwenda Jela na ikaonyesha mlango huu haukuwa wake baada ya kutoka akaachana na Udiwani na kurejea kwenye Muziki ambao ulimpokea japo haikuwa kwa ukubwa ule ambao aliutaka.

Hakukata Tamaa hakutaka kuendelea kuwa GUNDI aliamua kuufungua Mlango mwingine ambao ulikuwa ni kuongeza idadi ya Marafiki wa Faida na hapa alijikuta Mikononi mwa Mwanamuziki Nguli wa BONGOFLEVA Diamond Platnumz ambako huko hakuwa miongoni mwa Wasanii waliokuwa chini ya Lebo ya WCB bali yeye alikuwa ni CHAWA yaani mbeba Makoti wa Diamond Platnumz pamoja na kumsifia kwa kila kitu kiwe kizuri au kibaya kikubwa mkono uende kinywani, kwenye hili naweza kusema NYOTA ya Baba LEVO iliangaza vyema kwani alijikuta anapata kazi ya Utangazaji kwenye kituo cha Redio cha Wasafi, kama haitoshi akajikuta akisaini Mikataba mingi sana ya Ubalozi na Makampuni mengi ya Kibiashara kama vile SILENT OCEAN na KILIMANJARO CARGO ambako kafanya vizuri na kupelekea kufungua Kituo chake cha Online TV cha 7media ambacho kinafanya vizuri kutokana na Ubunifu wake hasa Upande wa kuandaa na Kusimamia Show za Ucheshi Wima.

Na sasa yuko kwenye hatua za mwisho kwenye Ujenzi wa Jumba lake la Kifahari. Hivyo ukiona haufii matarajio yako usiogope hata kidogo fanya maamuzi ya kufungua mlango wa pili na Kamwe usiwe Gundi, kwani utahangaika huku na kule kumtafuta Mchawi wa Maisha yako kumbe ni wewe mwenyewe.

Kwa leo Naishia hapa, kwenye episode inayokuja tutamuangalia Mtu mwingine aliyeamua kuchukua hatua ya Kufungua Mlango wa Pili wa Mafanikio.

Imeandikwa na Sultan Uwezo Tz

Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post